DIARRA AWANIA TUZO YA KIPA BORA AFRIKA DHIDI YA ONANA WA MAN UNITED


KİPA wa Yanga raia wa Mali, Djigui Diarra ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya  Kipa Bora Afrika akichuana na makipa wengine tisa baranı.
Hao ni Oussama Benbot wa USM Alger na Algeria, Andre Onana wa Cameroon na Manchester United, Yahia Fofana wa Angers na Ivory Coast, Lionnel Mpasi wa Rodez AF na DRC, Mostafa Shobeir wa Al Ahly na Mısri, Munir El Kajoui wa RS Berkane na Morocco, Stanley Nwabali Bobo wa Chippa United na Nigeria, Ronwen Williams wa Mamelodi Sundowns na Afrika Kusini na Amanallah Memmiche was Esperance na Tunisia.
Ni mara ya pili kwa Diarra kuingia kinyang’anyiro cha Tuzo huyo, ambayo mwaka jana ilichukuliwa na Yassine Bounou wa Morocco na Al Hilal.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA