NGORONGORO HEROES MABINGWA MICHUANO YA CECAFA U20


TANZANIA imetwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, CECAFA U20 baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya jioni hii Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Haukuwa ushindi mwepesi hata chembe, kwani Ngorongoro Heroes walilazimika kutoka nyuma baada ya Rising Stars kutangulia na bao la winga wa AFC Leopards, Kitsao Beja Hassan dakika ya 48.
Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Kocha mzoefu, Charles Boniface Mkwasa anayesaidiwa na Kally Ongala na Juma Kaseja Kocha wa makipa ikazinduka kwa mabao ya mshambuliaji wa Simba, Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 64 na kiungo wa Yanga, Shekhan Ibrahim Khamis dakika ya 82.
Ushindi ni sawa ni kısası cha mchezo wa kwanza wa Kundi A baina ya timu hizo ambao Kenya walishinda 2-1 piaz
Zote, Ngorongoro Heroes na Rising Stars zitaiwakilisha CECAFA katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) mwakani.
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Uganda iliichapa Burundi mabao 3-1 hapo hapo KMC Complex.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA