NIGERIA WAPEWA USHINDI DHIDI YA LIBYA KUFUZU AFCPON 2025


KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka (CAF) imeipa ushindi wa mabao 3-0 Nigeria dhidi ya Libya baada ya kuvunjika kwa mchezo wa Kundi D kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Mechi kati ya Libya na Nigeria haikufanyika Oktoba 15 mwaka huu baada ya Super Eagles kurejea nyumbani kufuatia madai ya kufanyiwa mambo yasiyo ya kiuanamichezo ikiwemo kuwekwa Uwanja wa Ndege m uda mrefu bila huduma yoyote.
Pamoja na Nigeria kupewa ushindi, lakini Shirikisho la Soka la Libya (LFF) limeamriwa kulipa faini ya Dola za kimarekani 50,000, ambayo wanatakiwa kulipa ndani ya siku 60 baada ya taarifa ya uamuzi huu.
"Shirikisho la Soka la Libya lilibainika kukiuka Kifungu cha 31 cha Kanuni za Jumla ya Nguvu za Kombe la Mataifa ya Afrika la CAF pamoja na Kifungu cha 82 na 151 cha Kanuni za Nidhamu za CAF,"imesema taarifa ya CAF leo.
Maamuzi hayo yanaifanya Nigeria ifikishe pointi 10 na kuendelea kuongoza Kundi A, ikifuatiwa na Benin pointi sita, Rwanda pointi tano na Libya inayoshika mkia kwa pointi yake moja baada ya wote kucheza mechi nne. 




Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA