SAMATTA AREJESHWA TAIFA STARS KWA AJILI YA MECHI DRC KUFUZU AFCON


KAIMU Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco amefanikiwa kumrejesha kikosini Nahodha Mbwana Ally Samatta ambaye alidhamiriwa kustaafu.
Morocco amemjumuisha kwenye kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco.
Taifa Stars watakuwa wageni wa DRC Alhamisi ya Oktoba 10 Uwanja wa Martyrs de la PentecĂ´te Jijini Kinshasa, kabla ya timu hizo kurudiana siku tano baadaye, Oktoba 15 Uwanja Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mara ya mwisho Samatta aliichezea Taifa Stars Januari 24, mwaka huu kwenye mechi ya Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 dhidi ya DRC Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo timu hizo zikitoka suluhu, 0-0 ambayo Samatta alimpisha Kokola Charles William M'Mombwa dakika ya 86.
Makipa; Ally Salim (Simba), Zuberi Foba (Azam FC), Yona Amos (Pamba), Mohamed Hussein (Pamba FC).
Mabeki; Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Pascla Msindo (Azam FC), Mohamed Hussein (Simba), Ibrahim Bacca (Yanga), Bakari Mwamyeto (Yanga), Dickson Job (Yanga), Abdulrazack Hamza (Simba), Haji Mnonga (Salford City, England),
Viungo; Adolf Mtasingwa (Azam FC), Habib Khalid (Singida Black Stars), Himid Mao (Taalal El Geish, Misri) Mudathir Yahya (Yanga), Faisal Salum, Suleiman Mwalimu, Cyrpian Kachwele (Vancouver Whitecaps, Canada).
Washambuliaji; Clement Mzizie (Yanga), Mbwana Samatta (PAOK FC), Kibu Dennis (Simba), NassOR Saadun (Azam FC) na Abdallah Said (KMC).  



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA