SIMBA NA YANGA ZAWANIA TUZO YA KLABU BORA AFRIKA


VIGOGO wa soka nchini, Simba na Yanga wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka Afrika baada ya kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
Watani hao wa hadi wanachuana na Al Ahly na Zamalek, zote za Mısri, Petro Atletico ya Angola, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Dreams FC ya Ghana, RS Berkane ya Morocco, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Esperance ya Tunisia.
Wakati Simba ilitolewa na Al Ahly ya Mısri kwa jumla ya mabao 3-0, ikifungwa 1-0 nyumbani na 2-0 ugenini - Yanga ilitolewa na Mamelodi Sundwons kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya jumla ya 0-0.
Al Ahly ndio walioibuka mabingwa baada ya kuichapa Esperance 1-0 ugenini na sare ya 0-0 nyumbani.
Katika Nusu Fainali Al Ahly iliitoa Mazembe ikiichapa 2-0 Cairo baada ya sare ya 0-0 Lubumbashi na Esperance iliitoa Mamelodi kwa jumla ya mabao 2-0 ikishinda 1-0 nyumbani na ugenini. 
Kwa Yanga huu ni mwaka wa pili mfululizo wanawania Tuzo hiyo ambayo mwaka jana ilichukuliwa na Al Ahly.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA