TANZANIA PRISONS YAICHAPA FOUNTAIN GATE 3-2 SOKOINE


TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Nurdin Chona kwa penalti dakika ya 25, Ezekia Mwashilindi dakika ya 48 na Vedastus Mwihambi dakika ya 50, wakati ya Fountain Gate yamefungwa na Suleiman Mwalimu dakika ya 12 na Kassim Suleiman dakika ya 37.
Kwa ushindi huo wa kwanza wa msimu, Tanzania Prisons inafikisha pointi saba katika mchezo wa sita, wakati Fountain Gate inabaki na pointi zake 13 za mechi saba sasa.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA