TUZO ZA CAF KUTOLEWA MARRAKECH DESEMBA 16 MWAKA HUU


TUZO za Shirikisho la Soka Afrika zitafanyika katika Jiji la kitalii, Marrakech nchini Morocco Desemba 16 mwaka huu 2024, taarifa ya CAF imesema.
Hii ni mara ya tatu mfululizo Morocco kuandaa sherehe hizo, baada ya kufanya tafrija nzuri iliyofana mwaka jana ikihusisha nyota wengi.
CAF itathibitisha muda wa kuanza kwa #CAFAwards24 kwa wakati ufaao.
Tuzo za Wanasoka Bora Afrika mwaka jana zote zilikwenda Nigeria, Victor Osimhen akishinda ya Wanaume na Asisat Oshoala akibeba ya wanawake.
Tuzo za CAF zinazingatia upekee kwa kiwango cha mchezaji, timu katika mashindano ya klabu na kitaifa na kuhitimisha kwa mataji.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA