DAR CITY, ABC KATIKA MCHUANO MKALI KUWANIA UBINGWA WA BETPAWA NBL 2024

Wachezaji wa mpira wa kikapu katika mechi tofauti za kuwania klabu bingwa ya Tanzania (betPawa NBL 2024) yanayo endelea kwenye uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.

TIMU ya mpira wa kikapu ya Dar City inaweza kutwaa ubingwa wa betPawa NBL endapo itaibuka na ushindi katika mchezo wa pili uliopangwa kufanyika usiku wa kesho, Novemba 19, 2024 kwenye Uwanja wa Chinangali Park, Dodoma.
Dar City wana nafasi kubwa ya ushindi baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo wa pointi 97-48 kwenye mechi ya kwanza. 
Katika mchezo huo, Dar City ilitawala kila robo ya mchezo, wakiongoza 29-16 kwenye robo ya kwanza, 15-13 kwenye ya pili, na 31-7 kwenye ya tatu, hali iliyowaacha ABC bila nafasi ya kurejea mchezoni. 
Timu hiyo ilihitimisha ushindi wao kwa 23-12 kwenye robo ya mwisho.
Dar City iliongozwa na wachezaji wake Shin Brownlee, Hasheem Thabeet Manka, Amin Mkosa, Gilbert Nijimbere, na Alinani Andrew ambao walionyesha uwezo wa hali ya juu na  kuiwezesha timu hiyo kukaribia kutwaa taji la betPawa NBL na kufuzu kushiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL) mwakani.
ABC, ambao wamefika fainali za NBL kwa misimu minne mfululizo, wanahitaji ushindi usiku wa leo ili kurejesha matumaini yao ya kutwaa taji.
 Historia yao ina mafanikio makubwa, ikiwemo ubingwa wa mwaka 2021 huko Arusha na nafasi ya pili ambapo, mwaka jana, walishindwa kutwaa taji hilo baada dhidi  JKT Stars huko Dodoma. 
Kwa upande wa wanawake, BD Lioness na Fox Divas wamefuzu fainali baada ya ushindi wa kuvutia katika mechi za nusu fainali. 
BD Lioness waliwashinda mabingwa watetezi Vijana Queens kwa alama 59-40, huku Fox Divas wakiibuka na ushindi wa 83-52 dhidi ya JKT Stars. 
Timu hizo zote mbili zinatazamia kutwaa taji kwenye fainali zijazo.
Akugumzia maendeleo ya michuano hiyo, Meneja wa Masoko wa Kanda ya Afrika Mashariki wa betPawa, Borah Ndanyungu alisema kuwa hamasa imekuwa kubwa hasa baada ya kuanzisha utaratibu wa kuwalipa wachezaji 12 na viongozi wanne kila mmoja sh140,000 endapo timu itashinda mechi.
 “Bonus hii imeongeza msisimko kwenye mashindano. Tunatarajia mchezo wa ushindani mkubwa usiku wa leo wakati wachezaji wa ABC wakijaribu kurejea na kudai zawadi hiyo,” alisema.
betPawa imetenga Sh milioni 130 kwa ajili ya zawadi, ikiwemo Sh milioni 14 za pesa taslimu za ushindi, huku kiasi kingine kikisaidia shughuli za utawala wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF). 
Wachezaji wa timu ya Vijana Queens ambao wanashiriki mashindano ya klabu bingwa ya mpira wa kikapu Tanzania (betPawa NBL 2024)  yanayoendelea kwenye uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.
Wachezaji wa mpira wa kikapu katika mechi tofauti za kuwania klabu bingwa ya Tanzania (betPawa NBL 2024) yanayo endelea kwenye uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.
Wachezaji wa Mvumi Rippers ya Dodoma  wakiwa katika picha ya pamoja. Timu hiyo ilishiriki mashindano ya kuwania klabu bingwa ya Tanzania (betPawa NBL 2024) ambbayo yanaendelea kwenye uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.
Mashabiki wakifuatilia mashindano ya kuwania klabu bingwa ya Tanzania  (betPawa NBL 2024)  ambayo yanaendelea kwenye uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya wanawake ya Fox Divas wakifuatilia mechi ya kuwania klabu bingwa ya Tanzania (betPawa NBL 2024) yanayo endelea kwenye uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TBF, Mwenze Kabinda, alisifu maandalizi mazuri ya mashindano hayo, akiwashukuru betPawa na wadhamini wengine kwa mchango wao.
Mechi ya usiku wa leo inatarajiwa kuwa na nishati ya hali ya juu na msisimko mkubwa wakati timu zote zinapopambana kutafuta ushindi kwenye fainali za NBL.



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA