DIARRA, SIMBA NA YANGA ZATUPWA NJE TANO BORA YA TUZO CAF 2024


KIPA wa Yanga na timu ya taifa ya Mali, Djigui Diarra kwa mara nyingine ameenguliwa kwenye orodha ya wachezaji watano wanaowani Tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka Afrika.
Diarra amezidiwa kete na Andre Onana wa Cameroon na Manchester United, Yahia Fofana wa Ivory Coast na Angers ya Scotland, Mostafa Shobeir wa Misri na Al Ahly, Stanley Nwabali wa Nigeria na Chippa United na Ronwen Wlliams wa Afrika Kusini na Mamelodi Sundowns.
Aidha, klabu za Simba na Yanga nazo zimetupwa nje kwenye orodha ya mwisho ya Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka Afrika zikizidiwa kete na Al Ahly na Zamalek za Misri, RS Berkane ya Morocco, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Esperance ya Tunisia.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) jana limetoa orodha kamili Tano Bora katika vipengele vyote vya Tuzo zake za Wanaume mwaka 2024 ambazo zitatolewa katika hafla itakayofanyika Desemba 16 Jijini Marrakech nchini Morocco.
Katika Tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika iliyoachwa wazi na mshindi wa mwaka jana, Victor James Osimhen anayecheza kwa mkopo Galatasaray ya Uturuki kutoka Napoli ya Italia Kipa wa Mamemldi, Ronwen Williams ndiye kipa pekee na mchezaji pekee anayecheza Afrika aliyeingia Tano Bora.
Anachuana na nyota wanaocheza Ulaya, Serhou Guirassy wa Guinea na Borussia Dortmund, Simon Adingra wa Ivory Coast na Brighton & Hove Albion, Achraf Hakimi wa Morocco na Paris Saint-Germain na Ademola Lookman wa Nigeria naAtalanta.
Ifuatayo ni orodha kamili ya walioingia Tano Bora ya Tuzo za CAF;
MWANASOKA BORA WA MWAKA
Simon Adingra (Cote d’Ivoire / Brighton & Hove Albion)
Serhou Guirassy (Guinea / Borussia Dortmund)
Achraf Hakimi (Morocco / Paris Saint-Germain)
Ademola Lookman (Nigeria / Atalanta)
Ronwen Williams (South Africa / Mamelodi Sundowns)
KIPA BORA WA MWAKA
Andre Onana (Cameroon / Manchester United)
Yahia Fofana (Cote d’Ivoire / Angers SCO)
Mostafa Shobeir (Egypt / Al Ahly)
Stanley Nwabali (Nigeria / Chippa United)
Ronwen Wlliams (South Africa / Mamelodi Sundowns)
MCHEZAJI BORA ANAYECHEZA AFRIKA
Issoufou Dayo (Burkina Faso / RS Berkane)
Ahmed Sayed ‘Zizo’ (Egypt / Zamalek)
Hussein El Shahat (Egypt / Al Ahly)
Mostafa Shobeir (Egypt / Al Ahly)
Ronwen Wlliams (South Africa / Mamelodi Sundowns)
KOCHA BORA WA MWAKA
Emerse Fae (Cote d’Ivoire)
Sebastien Desabre (DR Congo)
Marcel Koller (Al Ahly)
Hugo Broos (South Africa)
MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI WA MWAKA
Karim Konate (Cote d’Ivoire / Salzburg)
Oumar Diakite (Cote d’Ivoire / Reims)
Yankuba Minteh (Gambia / Brighton & Hove Albion)
Eliesse Ben Seghir (Morocco / AS Monaco)
Lamine Camara (Senegal / AS Monaco)
KLABU BORA YA MWAKA
Al Ahly (Egypt)
Zamalek (Egypt)
RS Berkane (Morocco)
Mamelodi Sundowns (South Africa)
Esperance Sportive de Tunis (Tunisia)
TIMU BORA YA TAIFA YA MWAKA
Cote d’ivoire
DR Congo
Nigeria
South Africa
Sudan


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA