JKT TANZANIA YAICHAPA PRISONS 1-0 MBWENI


BAO la kiungo Hassan Iddi Kapalata dakika ya pili limeipa JKT Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jénérali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 13 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya 10, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 10 za mechi 11 sasa nafasi ya 12.



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA