JKT TANZANIA YAWAKANDA FOUNTAIN GATE 1-0 PALE PALE KWARAA
BAO la kiungo mkongwe wa umri wa miaka 31, Najim Magulu dakika ya 34 limeipa JKT Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 16 na kusogea nafasi ya nane wakizidiwa tu wastani wa mabao na Mashujaa baada ya wote kucheza mechi 11, wakati Fountain Gate inabaki na pointi zake 17 za mechi 12 sasa nafasi ya sita.
Comments
Post a Comment