TABORA UNITED YATOKA NYUMA KUTOA SARE NA SINGIDA 2-2 MWINYI


WENYEJI, Tabora United wametoka nyuma na kupata sare ya 2-2 na Singida Black Stars katika mchezo wa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara asuhuhi ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Singida Black Stars walitangulia kwa mabao ya mshambuliaji Mkenya, Elvis Baranga Rupia dakika ya 16 na beki Muivory Coast, Anthony Urbain Tra Bi Tra dakika ya 32, kabla ya Tabora United kukomboa kupitia kwa washambuliaji wa zamnai wa Yanga, Yacouba Sogne dakika ya 45’+1 na Mkongo, Heritier Ma Olongi Makambo dakika ya 49.
Kwa matoke ohayo, Tabora United inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya tano, ikizidiwa pointi sita na Singida Black Stars ambayo hata hivyo ina mchezo mmoja mkononi.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA