YANGA SC YAENDELEA KUBORESHA BENCHI LA UFUNDI
KLABU ya Yanga imeendelea kuimarisha Benchi lake la Ufundi kwa kutambulisha Maafisa wawili wapya, Mmarekani mwenye asili ya Somalia, Abdihamid Mohamed Moallin anayekuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Msaidizi, Mustafa Kodro raia wa Bosnia-Herzegovina.
Hatua hiyo inakuja siku mbili baada ya mabingwa hao wa Tanzania kumtambulisha Kocha mpya, Mjerumani mwenye asili ya raia wa Bosnia-Herzegovina, Sead Ramovic kutoka TS Galaxy ya Afrika Kusini akichukua nafasi ya Muargentina, Miguel Angel Gamondi aliyeondolewa Ijumaa.
Abdihamid Mohamed Moallin (35) anatua Yanga akitokea KMC ya Kinondoni baada ya awali kufundisha Azam FC kote akiwa Kocha Mkuu, wakati Mustafa Kodro (43) anatokea TS Galaxy ya Afrika Kusini alipokuwa Msaidizi wa Ramovic tangu Desemba mwaka 2022.

Moallin alianzia kufundisha Columbus Crew ya Marekani kama Kocha Msaidizi na baadaye Horseed ya Somalia Kocha Mkuu, kabla ya kuja Tanzania mwaka 2021.
Mustafa Kodro alianzia kwenye kucheza kandanda kama kiungo wa ulinzi akichezea klabu mbalimbali kwao, kabla ya kustaafu mwaka 2016 na kuingia kwenye Ukocha akianzia Velez Mostar mwaka 2019, baadaye FK Sarajevo Juni mwaka 2022 kabla ya Desemba kutua TS Galaxy.
Comments
Post a Comment