ATEBA APIGA ZOTE MBILI SIMBA SC YAICHAPA KEN GOLD 2-0 MWENGE


TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ken Gold ya Mbeya 
katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mabao yote ya Simba SC leo yamefungwa na mshambuliaji wake Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida dakika ya 34 kwa penalti na dakika ya 44 akimalizia kazi nzuri ya beki Mburkinabe, Valentin Nouma.
Kwa ushindi huo, Simba inayofundishwa kocha raia wa Afrika Kusini Fadlu Davids inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 12, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na Azam FC, ambayo pia imecheza mechi tatu zaidi.
Kwa upande wao Ken Gold walio chini ya Kocha Omar Kapilima hali inazidi kuwa mbaya wakikamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza mkiani, wakibaki na pointi zao sita.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA