AZAM FC YAWACHAPA IRINGA 4-0 KOMBE LA TFF CHAMAZI


WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kutinga Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Michuano inayodhaminiwa na benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Iringa SC leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Mkongo, Yanick Litombo Bangala dakika ya 25, beki Mcolomboa, Yeison David Fuentes Mendoza dakika ya 45’+1, Sospeter Bajana dakika ya 65 na Daud Said dakika ya 74.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA