COASTAL UNION YAAMBULIA SARE KWA KMC, 1-1 ARUSHA


WENYEJI, Coastal Union wametoka sare ya kufungana bao 1-1 na KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
KMC walitangulia kwa bao la mapema tu dakika ya kwanza, kabla ya Maulid Juma kuisawazishia Coastal Union kwa penalti dakika ya 89.
Kwa matokeo hayo, Coastal Union inafikisha pointi 18, ingawa inabaki nafasi ya 11 ikizidiwa pointi moja na KMC baada ya wote kucheza mechi 16 sasa.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA