DODOMA JIJI FC YAIKUNG’UTA MASHUJAA 3-1 JAMHURI
WENYEJI, Dodoma Jiji wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na Mwana David Kibuta dakika ya 12, Lulihoshi Heritier dakika ya 16 na Zidane Sereri dakika ya 83, wakati la Mashujaa limefungwa na Crispin Ngushi dakika ya 90 na ushei.
Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya tisa, ikizidiwa tu wastani wa mabao na Mashujaa na JKT Tanzania baada ya wote kucheza mechi 16.
Comments
Post a Comment