JKT TANZANIA YASONGA MBELE KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHAPA IGUNDA UTD 5-1


TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kwenda Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Igunga United jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Wilson Nangu dakika ya 12, Nahodha John Bocco dakika ya 14, Mohamed Bakari mawili dakika ya 16 na 30 na Danny Lyanga dakika ya 68, wakati bao pekee la Igunga United limefungwa Joel Loya dakika ya 58. 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA