KAGERA SUGAR YAAMBULIA SARE KWA NAMUNGO, 1-1 KAITABA


WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Mabao yote yalifungwa na viungo washambuliaji, Hassan Salum Kabunda akianza kuifungia Namungo dakika ya 60, kabla ya Mganda Peter Lwasa kuisawazishia Kagera Sugar dakika nne baadaye.
Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi 14 katika mchezo wa 11 na inabaki nafasi ya 14, wakati Namungo FC inafikisha pointi 10 katika mchezo wa 13, nayo inabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA