MJUMBE BODI YA WAKURUGENZI AZAM FC AFIWA NA BABA YAKE MZAZI


MJUMBE was Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC, Careen Bahadour amefiwa na baba yake mzazi, Mzee Marhun Shermohamed 'Sheru' jana Jumatatu nchini Afrika Kusini alipokuwa anafanyiwa matibabu.
Taarifa ya Azam FC mapema leo umesema kwamba mazishi yanafanyika Saa 4:00 asubuhi ya leo kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam baada ya Sala itakayofanyika msikiti wa Maamur, Upanga,
“Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia ya @careem99_, ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huu,”imesema taarifa ya Azam FC mapema leo.
Inna Lillahi Wainna Ilaihi Rajiun! 🙏🙏🙏


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA