NAMUNGO FC YAICHAPA FOUNTAIN GATE 2-1 PALE PALE BABATI


TIMU ya Namungo FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati mkoani Manyara.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na viungo Pius Charles Buswita dakika ya 10 na Geoffrey Julius Luzendaze dakika ya 78, wakati bao pekee la Fountain Gate limefungwa na winga Salum Kihimbwa dakika ya 30.
Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 16 na kusogea nafasi ya 11, wakati Fountain Gate wanabaki na pointi zao 20 za mechi 15 sasa nafasi ya sita.  


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA