NAMUNGO FC YATOKA NYUMA KWA MABAO MAWILI NA KUICHAPA KEN GOLD 3-2 SOKOINE


TIMU ya Namungo FC imetoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda 3-2 dhidi ya wenyeji, Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Ken Gold walitangulia kwa mabao ya Mishamo Daudi dakika ya pili na Joshua Ibrahim dakika ya tisa, kabla ya Namungo kuzinduka kwa mabao ya mkongwe, Erasto Nyoni dakika ya 24 kwa penalti na 90’+3 na Fabrice Ngoy dakika ya 36.
Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 13 na kusogea nafasi ya 12 kutoka ya 15, wakati Ken Gold inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 ikibaki na pointi zake sita baada ya timu zote kucheza mechi 14.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA