PAMBA JIJI YAILAMBA KEN GOLD KIDUDE KIRUMBA SHUGHULI YA MPOLE


BAO pekee la mshambuliaji George Mpole Mwaigomole dakika ya 72 limeipa Pamba Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Kwa ushindi huo, Pamba Jiji inafikisha pointi 11 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya 13, wakati Ken Gold inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 ikibaki na pointi zake sita za mechi 13 pia.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu iliyopangwa kuchezwa jioni ya leo baina ya Coastal Union na Tanzania Prisons imeahirishwa kutokana na Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kujaa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Jijini Arusha.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA