SERENGTI BOYS YACHAPWA 2-1, UGANDA NDIO MABINGWA CECAFA U17
WENYEJI, Uganda wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (CECAFA U17) baada ya kuichapa Tanzania mabao 2-1 leo Uwanja wa Hamz, Nakivubo Jijini Kampala.
Tanzania waliuanza vyema mchezo huo na kupata bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa Abel Josiah, kabla ya Uganda kuzinduka kipindi cha pili na kufunga mabao mawili kupitia kwa Arafat Nkoola na James Bogere.
Uganda na Tanzania wote wamefuzu Fainali za Afrika, AFCON U17 ambazo zitafanyika mwakani nchini Morocco.
Comments
Post a Comment