TABORA UNITED YAAMBULIA SARE KWA COASTAL UNION, 1-1 ‘KWA MWINYI’


WENYEJI, Tabora United wamepunguzwa kasi baada ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Costal Union ilitangulia kwa bao la Jeremier Ntabwe dakika ya Dk 45’+2, kabla ya Banele Junior kuisawazishia Tabora United dakika ya 56.
Kwa matokeo hayo, Tabora United inafikisha pointi 25, ingawa inabaki nafasi ya tano na Coastal Union inafikisha pointi 17, nayo inabaki nafasi ya 10 kwenye ligi ya timu 16.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA