TANZANIA PRISONS YAICHAPA PAMBA JIJI 1-0 UWANJA WA SOKOINE


TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Pamba Jiji ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Tariq Abdallah Simba aliyefumua shuti la umbali wa mita 17 kumtungua kipa wa zamani wa Tanzania Prisons, Yona Geoffrey Amos dakika ya 31.
Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons wanafikisha pointi 14 na kujiinua hadi nafasi ya 13, ikiishushia Pamba Jiji nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi 16. 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA