ZUBERI FOBA MASUDI AONGEZA MKATABA AZAM FC HADI 2027


KLABU ya Azam imemuongeza mkataba wa miaka miwili kipa wake wa pili, Zuberi Foba Masudi ambao utamfanya aendelee kuitumikia timu ya Bilionea Alhaj Sheikh Salim Bakhresa na familia yake hadi mwaka 2027.
“Kipa wetu @foba_zubeir, ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2027 baada ya kuongeza mkataba mpya wa miaka miwili,”umesema taarifa ya Azam FC leo.
Licha ya kuwa kipa wa pili nyuma ya Mustafa Mohamed wa Sudan, lakini Foba amekuwa na mwendelezo mzuri msimu huu akiwa amedaka mechi tano za mashindano yote bila kuruhusu bao hata moja.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA