CAF YASOGEZA MBELE FAINALI ZA CHAN ILI MAANDALIZI YAKAMILIIKE VIZURI


SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) jana lilitangaza kuahirisha Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Kenya, Tanzania na Uganda  hadi Agosti 2025.
Taarifa ya CAF ilisema wenyeji, Kenya, Tanzania na Uganda wamefanikisha vizuri zoezi la ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya kufanyia mazoezi, hoteli, hospitali na miundombinu na vifaa vingine kwa ajili ya kuandaa Fainali za CHAN.
Hata hivyo, wataalam wa Ufundi na Miundombinu wa CAF ambao baadhi yao wamejikita katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda, wameishauri CAF kuwa muda zaidi unatakiwa kuhakikisha miundombinu na vifaa viko katika viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kufanya CHAN yenye mafanikio.
Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe alisema: “Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea na maendeleo mazuri yaliyofikiwa katika kujenga na kuboresha viwanja, viwanja vya kufanyia mazoezi, hoteli, hospitali na miundombinu na vifaa vingine nchini Kenya, Tanzania na Uganda kwa ajili ya kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies (CHAN) Kenya, Tanzania, Uganda 2024,". 
"Nimefurahishwa na ujenzi na ukarabati unaoendelea wa miundombinu na vifaa vya mpira wa miguu nchini Kenya, Tanzania na Uganda. Nina imani kuwa viwanja, viwanja vya mazoezi, hoteli, hospitali na miundombinu na vifaa vingine vitakuwa katika viwango vinavyohitajika vya CAF kwa kuandaa, Agosti 2025, Mashindano ya Jumla ya Nishati ya Afrika ("CHAN") yenye mafanikio makubwa Kenya, Tanzania, Uganda 2024,”.
Pamoja na kuahirisha Fainali hizo, lakini CAF imesema zoezi la kufanya Droo ya CHAN itafanyika kama kawaida leo Jijini Nairobi, kuanzia Saa 2:00 usiku na tarehe mpya ya kuanza kwa Fainali hizo  itatajwa baadaye.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA