KILIMANJARO STARS YATOLEWA MAPEMA KOMBE LA MAPINDUZI PEMBA


TIMU ya Tanzania Bara imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Kenya leo Uwanja wa Gombani, Pemba, Zanzibar.
Mabao ya Harambee Stars yaliyoizamisha Kilimanjaro Stars yamefungwa na Boniphace Muchiri dakika ya 56 na Ryan Ogam dakika ya 68.
Kwa ushindi huo, Harambee Stars inafikisha pointi nne, sawa na Burkina Faso, zikifuatiwa na wenyeji, Zanzibar Heroes yenye pointi tatu, wakati Tanzania Bara haina lolote wala chochote baada ya timu zote kucheza mechi mbili mbili.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA