SIMBA KUIKABILI CS CONSTANTINE UWANJA MTUPU BILA MASHABIKI

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeifingia klabu ya Simba kuingiza watazamaji katika mechi zake mbili za Kombe la Shirikisho Afrika baada ya vurugu zilizotokea kwenye mechi dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia Desemba 15, 2024 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Siku hiyo, Simba SC ilitoka nyuma na kushinda 2-1 kabla ya vurumai kuibuka na mashabiki wake kushambuliana na mashabiki wa wageni kwa kurushiana viti walivyokuwa wanang’oa uwanjani.
Maana yake Simba hawatakuwa na watazamaji katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi A Kombe la Shirikisho dhidi ya CS Constantine Jumapili.



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA