SIMBA SC YAICHAPA SFAXIEN 1-0 TUNISIA BAO LA AHOUA
TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, CS Sfaxien katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Olympique Hammadi-Agrebi mjini Radès nchini Tunisia.
Bao pekee la Simba katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast Jean Charles Ahoua dakika ya 34.
Kwa ushindi huo, Simba SC imefikisha pointi tisa na kupanda kileleni mbele ya Bravos do Marquis ya Angola na CS Constantine ya Algeria zenye pointi sita kila moja, wakati CS Sfaxien inabaki mkiani kwa rekodi ya kupoteza mechi nne, mbili nyumbani na mbili ugenini.
Comments
Post a Comment