SIMBA SC YAWATANDIKA WAALGERIA 2-0 KIBU NA ATEBA
WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya CS Constantine ya Algeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na kiungo mzawa, Kibu Dennis Prosper dakika ya 61 na mshambuliaji Mcameroon Christian Leonel Ateba Mbida dakika ya 79.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 13 na kumaliza kileleni mwa kundi hilo, mbele ya CS Constantine yenye pointi 12 na zote zimefuzu Robo Fainali.
Mechi nyingine ya Kundi A Kombe la Shirikisho leo wenyeji, CS Sfaxien wameichapa Bravos do Maquis Uwanja wa Olimpiki Hammadi-Agrebi mjini Radès, Tunisia.
Pamoja na kipigo cha leo Bravos do Maquis wamemaliza nafasi ya tatu kwa pointi zao saba, huku Sfaxien yenye pointi tatu imeshika mkia.
Comments
Post a Comment