TANZANIA YAPANGWA KUNDI LA KAWAIDA CHAN, KENYA SHUGHULI WANAYO, UGANDA…


WENYEJI wenza, Tanzania wamepangwa Kundi B katika Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN)  pamoja na Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).
Katika droo iliyofanyika usiku wa leo ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya – wenyeji wenza wengine, Kenya wamepangwa Kundi B pamoja na mabingwa mara mbili wa CHAN, Morocco, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na  Zambia.
Wenyeji wenza wengine, Uganda wamepangwa Kundi C pamoja na Niger, Guinea na timu nyingine mbili zitakazojulikana baadaye na Kundi D linazikutanisha Senegal, Kongo-Brazzaville, Sudan na Nigeria.
Droo hiyo iliondeshwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF,) Samson Adamu aliyesaidiwa na wachezaji wastaafu, McDonald Mariga wa Kenya, Mrisho Ngasa wa Tanzania na Hassan Wasswa wa Uganda.
Michuano hiyo ya nane ya awali ilikuwa ifanyike Februari, lakini imesogezwa mbele hadi Agosti ili kutoa fursa kwa wenyeji kumalizia kazi yao nzuri ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu.
 Viwanja vitakavyotumika kwa Fainali hizo ni Benjamin Mkapa, Dar es Salaam unaoingiza watazamaji 60,000 na Amaan, Zanzibar wenye kuchukua watazamaji 20,000), Mandela wa Kampala unaomeza watu 45,000— na Nyayo unaokusanya watu 18,000 na  Moi International Sports Centre wenye kubeba watazamaji 55,000 vyote vya Nairobi.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA