YANGA WAIKOSA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA
SAFARI ya Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika imeishia hatua ya 16 Bora baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi A kufuatia sare ya bila mabao na MC Alger katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Yanga ilihitaji ushindi leo ili kufuzu kwa mara ya pili mfululizo Robo Fainali, lakini mpango mzuri wa kujilinda wa MC Alger na papara za wachezaji wake kila walipopata nafasi ziliwanyima mabao wenyeji.
Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi A leo, wenyeji TP Mazembe wameibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Al Hilal Omdurman Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa matokeo hayo, Al Hilal Omdurman imemaliza kileleni na pointi zake 10, ikifuatiwa na MC Alger pointi tisa na zote zimefuzu Robo Fainali, wakati Yanga yenye pointi nane na Mazembe pointi tano zote zimeaga.
Comments
Post a Comment