YANGA YAFUNGA DIRISHA DOGO KWA USAJILI WA JONATHAN IKANGALOMBO KAPELA



KLABU ya Yanga imemtambulisha winga wa kulia, Jonathan Ikangalombo Kapela kutoka AS Vita Club ya kwao, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa mchezaji wake mpya wa pili dirisha hili dogo.
Anamfuatia beki wa kulia, Israel Patrick Mwenda anayeweza kucheza kama winga wa kulia pia na kiungo, aliyesajiliwa kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu kutoka Singida Black Stars.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA