ZANZIBAR HEROES YACHAPWA 1-0 NA BURKINA FASO KOMBE LA MAPINDUZI


WENYEJI, Zanzibar usiku wa Jumatatu wamechapwa bao 1-0 na Burkina Faso katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Uwanja wa Gombani, Pemba, Zanzibar.
Bao pekee la The Stallions lililoizamisha Zanzibar Heroes usiku wa jana lilifungwa na Hanabi Hadalou dakika ya 74 na sasa Burkina Faso inaongoza ligi ya michuano hiyo kwa pointi zake nne kuelekea mechi yake ya mwisho na Tanzania Bara.
Zanzibar Heroes wanabaki nafasi ya pili kwa pointi zao tatu walizovuna kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya ndugu zao, Kilimanjaro Stars kwenye mchezo wa ufunguzi.
Michuano hiyo inaendelea leo kwa mchezo mwingine mmoja, Tanzania  Bara dhidi ya jirani zao, Kenya.
Wakati Kilimanjaro Stars ilichapwa 1-0 na Zanzibar Heroes kwenye mechi ya ufunguzi — Harambee Stars waliƂazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na The Stallions.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA