ZANZIBAR HEROES YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI, HARAMBEE STARS ‘OUT’


WENYEJI, Zanzibar wamefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya usiku huu Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Bao pekee la Zanzibar Heroes lililokatisha safari ya Harambee Stars kwenye michuano hiyo iliyoshirikisha timu nne limefungwa na Ali Khatib ‘Inzaghi’ dakika ya 90’+3 akimalizia kazi nzuri ya Nahodha, Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Timu zote mbili zilimaliza pungufu baada ya wachezaji wawili kutolewa kwa kadi nyekundu, Abdu Omar wa Harambee Stars dakika ya 68 na Ibrahim Ame wa Zanzibar Heroes dakika ya 90’+9.
Kwa ushindi huo, Zanzibar Heroes inafikisha pointi sita na kumaliza nafasi ya pili, nyuma ya Burkina Faso yenye pointi saba na Kenya pointi nne, wakati Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imetoka patupu kufuatia kufungwa mechi zote tatu.
Sasa Burkina Faso na Zanzibar zitakutana katika mchezo wa Fainali Jumatatu hapo hapo Uwanja wa Gombani. 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA