KOCHA MPYA YANGA AMEFUNDISHA UFARANSA, KUWAIT, SAUDI ARABIA, MOROCCO NA KLABU KUBWA ALGERIA
KOCHA mpya wa Yanga, Miloud Hamdi (53), Mualgeria mwenye uraia wa Ufaransa ana uzoefu wa kufundisha soka tangu mwaka 2004 alipoanza na timu ya vijana nchini Ufaransa, ES Vitrolles, kabla ya kuhamia GS Consolat mwaka 2009 hadi 2012 .
Baada ya hapo akaenda Ettifaq U21 ya Saudi Arabia hadi mwaka 2015
USM Alger akaajiriwa kama Kocha Msaidizi wa USM Alger ya Algeria, kabla ya kupewa Ukocha Mkuu mwaka 2016.
Baadaye mwaka 2016 akaenda Nahdat Berkane ya Morocco, kabla ya kurejea USM Alger mwaka 2017 hadi 2018 akaenda Al-Salmiya SC ya Kuwaiti, kabla ya kurejea Algeria mwaka 2021 kufundisha CS Constantine hadi 2022 alipohamia JS Kabylie hadi mwaka jana.
Anajiunga na Wananchi kuchukua nafasi ya Siad Ramovic mwenye uraia wa Ujerumani aliyeondoka ghafla jana.
Comments
Post a Comment