PAMBA JIJI YAICHAPA DODOMA JIJI 1-0 PALE PALE JAMHURI


BAO pekee la mshambuliaji Mkenya, Mathew Tegisi Momanyi dakika ya 23 limetosha kuipa Pamba Jiji FC ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Kwa ushindi huo, Pamba Jiji inafikisha pointi 15 katika mchezo wa 17, japokuwa inabaki nafasi ya 14 na Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 19 za mechi 17 nafasi ya tisa.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA