PRINCE DUBE MCHEZAJI BORA LIGI KUU FEBRUARI, HAMDI KOCHA BORA
KLABU ya Yanga imeshinda Tuzo za Kocha Bora na Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Februari mwaka huu.
Mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo amewashinda mchezaji mwenzake wa Yanga, kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki na mshambuliaji wa Kengold, Suleiman Salim Rashid 'Bwenzi' kutwaa Tuzo hiyo.
Kwa upande wake Kocha Mualgeria wa Yanga, Miloud Hamdi amewashinda Muafrika Kusini, Fadlu Davids wa Simba na mzawa, Freddy Felix Minziro wa Pamba Jiji.
Comments
Post a Comment