AZAM FC YATOKA NYUMA NA KUICHAPA KAGERA SUGAR 4-2 KAITABA


TIMU ya Azam FC imetoka nyuma na kushinda mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na beki Lusajo Elukaga Mwaikenda dakika ya 42, winga Iddi Suleiman Ally  'Nado' dakika ya 58, kiungo Nassor Yahya Kapama aliyejifunga dakika ya 83 na mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco Yus dakika ya 87.
Kwa upande wa wenyeji, Kagera Sugar walipata mabao yao kupitia kwa wachezaji wa nafasi ya kiungo Hija Shamte Lidah dakika ya na 26 na Kassim Ibrahim Feka dakika ya 61.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 54 na kurejea nafasi ya tatu ikiizidi pointi moja Singida Black Stars baada ya wote kucheza mechi 27, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 22 za mechi 27 pia nafasi ya 15.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NI YANGA BINGWA KOMBE LA MUUNGANO 2025