KOCHA MMOROCCO WA AZAM FC ALIMWA FAINI KWA KUWAFANYIA FUJO MAREFA
KOCHA wa Azam FC, Mmorocco Rachid Taoussi ametozwa Faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kuwafanyia fujo na kuwarushia chupa marefa katika dhidi na ya wenyeji, Singida Black Stars Aprili 6 Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
Rachid Taoussi aliye katika msimu wake wa kwanza Azam FC amedaiwa kufanya hayo baada ya mchezo huo ambao timu yake ilichapwa 1-0, bao pekee la mshambuliaji Mkenya, Elvis Baranga Rupia dakika ya 75.
Comments
Post a Comment