MTIBWA SUGAR YAREJEA LIGI KUU BAADA YA MSIMU MMOJA TU TANGU ISHUKE


TIMU ya Mtibwa Sugar imejihakikishia kurejea Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya msimu mmoja tu licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na Big Man FC  jana Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Matokeo hayo yanaifanya Mtibwa Sugar ifikishe pointi 67 katika mechi ya 28, ambazo ni Mbeya City pekee inaweza kufikisha ikiwa itashinda mechi zake zote mbili za mwisho – hivyo imejihakikishia kuwa moja ya timu mbili zinazopanda Ligi Kuu.
Big Man inabaki na pointi zake 46 nafasi ya saba ikiwa bado kwenye mawindo ya kupanda Ligi Kuu kupitia Play-Off.
 




Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA