SIMBA SC KUONDOKA NA WACHEZAJI 23 KESHO KUIFUATA STELLENBOSCH
KIKOSI cha Simba SC cha wachezaji 23 kinatarajiwa kuondoka kesho asubuhi kwenda Jijini Durban, Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Stellenbosch Jumapili.
Simba SC inahitaji sare ya aina yoyote kukata tiketi ya Fainali baada ya ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Jumapili ya juzi Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Kimataifa wa Ivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 45'+2 kwa shuti la kitaalam la mpira wa adhabu lililomshinda kipa wa Afrika Kusini, Oscarine Masuluke.
Mechi ya marudiano itaanza Saa 10:00 jioni pia Uwanja wa Moses Mabhida Jijini Durban na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla Kati ya RSB Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria katika Fainali.
Ikumbukwe ilishinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza mabao ya Youssef Mehri dakika ya kwanza, Msenegal, Paul Valère Bassène dakika ya 21 na Oussama Lamlaoui, mawili dakika ya 54 na 90'+2 Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Morocco.
Comments
Post a Comment