TANZANIA MABINGWA TENA MICHUANO YA SHULE ZA AFRIKA WAVULANA
TANZANIA imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Michuano ya Ubingwa wa Shule za Afrika (ASFC), inayoshirikisha vijana chini ya umri wa miaka 15 kwa mara ya pili mfululizo baada ya ushindi wa Penalti 3-2 dhidi ya Senegal kufuatiua sare ya bila mabao jana Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ghana Jijini Accra.
Hiyo inakuwa mara ya pili mfululizo kwa vijana hao wa Tanzania kutwaa taji hilo baada ya mwaka jana pia kuwa mabingwa visiwani Zanzibar.
Upande wa wanawake, wenyeji Ghana waliweka heshima baada ya kutwaa ubingwa kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Uganda.
Michuano hiyo iliyofanyika kwenye viwanja Chuo Kikuu cha Ghana kuanzia Aprili 23 hadi 26 ilikutanisha vijana wenye vipaji bora kutoka kote barani Afrika, kusherehekea ubora, umoja na nguvu ya mabadiliko ya soka.
Sherehe za kufunga mashindano hayo ya siku nne yanayofanyika kwa msimu wa tatu mfululizo zilihudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dk Patrice Motsepe na Mkuu wa Nchi ya Ghana, Rais John Dramani Mahama ambao kwa pamoja walikabidhi mataji kwa timu zote mbili.
Kwa Wavulana Ghana walifanikiwa kutwaa nafasi ya tatu baada ya kuifunga Uganda, huku mabingwa wa zamani kwa Wasichana, Afrika Kusini walipata medali ya shaba baada ya kuishinda Morocco 2-1.
WASHINDI WA TUZO ZA MICHUANO HIYO
WASICHANA:
Mfungaji Bora: Pulane Moloi (Afrika Kusini)
Kipa Bora: Precious Akenguwie (Ghana)
Mchezaji Bora: Jennifer Awuku (Ghana)
Timu ya Kiungwana: Morocco
WAVULANA:
Mfungaji Bora: John Andor (Ghana), Ingatus Cyril Acquah Hagan (Ghana)
Mchezaji Bora: Souleymane Commissaire Faye
Kipa wa Bora: Rajabu Manyelezi (Tanzania)
Timu ya Kiungwana: Tanzania
Comments
Post a Comment