TANZANIA YAANZA VIBAYA AFCON U20, YACHAPWA 1-0 NA AMAJITA


TANZANIA imeanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika  kwa vijana chini ya Umri wa miaka 20 baada ya kuchapwa bao 1–0 na Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa  Suez Canal Jijini Ismailia nchini Misri inakofanyika michuano hiyo.
Bao pekee la Amajita lililoizamisha Ngorongoro Heroes limefungwa na Shakeel April wa Cape Town City dakika ya 27 akimalizia kazi nzuri ya Mogamat Faiz Abrahams wa Stellenbosch, wote viungo.
Ngorongoro Heroes itashuka tena dimbani Mei 3 kumenyana na  Sierra Leone, kabla ya kucheza na Zambia Mei 6 na kukamilisha mechi zake za Kundi A Mei 9 kwa kumenyana na wenyeji, Misri. 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NI YANGA BINGWA KOMBE LA MUUNGANO 2025