TANZANIA YACHAPWA 3-2 NA MOROCCO FAINALINYA FUTSAL AFRIKA


TANZANIA jana imefungwa mabao 3-2 na wenyeji, Morocco katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya Futsal kwa Wanawake Afrika Uwanja wa Salle Moulay Abdellah Jijiji Rabat.
Mabao ya Morocco yalifungwa na El Madani dakika ya 19, Korrych dakika ya  33 na Demraoui dakika ya 39, wakati ya Tanzania yalifungwa na Anastasia Antony Katunzi dakika ya tatu na na Jamila Rajab Mnunduka dakika ya 15.


Kipa wa Tanzania, Naijat Idrisa Bakari alichaguliwa mchezaji bora baada ya mchezo huo wa Fainali.
Pamoja na kufungwa katika mchezo wa Fainali, Tanzania nayo imeumgana na Morocco kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Futsal zitakazofanyika nchini  Philippines kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 7, mwaka huu.



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA