YANGA YAWAADABISHA TABORA UNITED, YAWACHAPA 3-0 MWINYI


MABINGWA watetezi, Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mabao ya Yanga yamefungwa na beki wazawa, Israel Patrick Mwenda dakika ya 21, Clement Francis Mzize dakika ya 57 na Mzimbabwe, Prince Mpumelelo Dube dakika ya 68, wote washambuliaji.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 61 katika mchezo wa 23 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya jirani zao, Simba ambao pia wana mechi moja mkononi.
Kwa upande wao Tabora United baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 37 za mechi 24 sasa nafasi ya tano.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA