BODI YATOA RATIBA MPYA; SIMBA NA YANGA NI JUNI 15 ‘KWA MKAPA’

BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetoa ratiba ya kukamilisha msimu huku mchezo wa watani wa jadi, Simba SC na Yanga ukipangwa kufanyika Juni 15 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika Machi 8, lakini Simba wakagoma kwa madai walizuia na wenyeji, Yanga kufanya mazoezi Uwanja wa Mkapa siku moja kabla ya mechi kwa muiibu wa kanuni.


Yanga iliandika malalamiko TPLB ikiomba ipewe ushindi baada ya Simba kutotokea uwanjani — na baadaye wakapeleka malalamiko Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) wakiomba pia wapewe ushindi.
Lakini FIFA na CAS wakaitaka kwanza Yanga ianzie kwenye mamlaka za nchini — lakini jana klabu hiyo imetoa taarifa ya kusistiza kutocheza mechi hiyo kwa sababu hawana imani na mamlaka za nchini.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA