YANGA SC YATINGA FAINALI KOMBE LA CRDB


MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 41 na kiungo mzawa, Mudathir Yahya Abbas dakika ya 89.
Yanga sasa itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili, Singida Black Stars na Simba zitakazomenyana baadaye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara. 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA